SEHEMU YA 4
ILIPOISHIA….
KATIKATI ya mduara huo niliona msichana mrembo sana. Yaani mzuri wa ajabu.
Alivaa nguo nyeupe za Hariri. Alijisitiri mwili mzima na alisimama mbele yangu hatua chache kutoka nipokuwa nimekaa.
Aliachia tabasamu pana katika uso wake mzuri na kunyoosha mikono yake kama vile anayeniita.
“Chriss,”aliniita tena.
“Wewe ninani na unataka nini kwangu?” nilimuuliza huku nikimshangaa.
MTUNZI: CHRISTOPHER LISSA
ISBN ….978-9987-9886-1-7
(Toa maoni ya simulizi hii 0654 58 67 88, 0629 643 419)
SASA ENDELEA…
“MH!!Mimi ni malaika?”
“Malaika?” nilihoji.
“Ndiyo! Malaika”
“Malaika wa Mungu au malaika wa shetani?” niliomhoji huku nikisimama.
Ulipita ukimya kidogo! Yule msichana akabetua macho yake na kunitazama kwa umakini. Akaachia tabasamu pana.
“Malaika wa kuzimu,” akanijibu.
“Kuzimu!!?
“Ndiyo! Kuzimu,”
“Kwa hiyo wewe ni Malaika wa Shetani?”
Hakunijibu…
“Unataka nini kwangu?”nikamuuliza.
“Chriss! Wewe umechaguliwa. Wewe umechaguliwa maalumu ”
“Nimechaguliwa? Nimechaguliwa na nani?”
“Umechaguliwa na Mkuu”
“Mkuu? Mkuu gani!?”
“Mkuu wetu wa kuzimu”
“Shetani!!?” nikamaka kwa mshituko.
Hakunijibu tena…
“Nichaguliwe kwa lipi?”
“Kuna kazi anataka kukupa,”
“Kazi!!? Kazi gani!!?”
“Mkuu anakuhitaji. Atakueleza kazi ya kufanya ukifika kuzimu,”
“Nikifika kuzimu!!?”
“Ndiyo! Mi nimewkuja kukuchukua utapewa maelezo tukifika kuzimu” alijibu
“Mimi siko tayari! Siko tayari tena uondoke hapa mara moja. Siko tayariii,” nilijibu kwa hamaki..
“Sikiliza Chriss, ili kazi hiyo ikamilike lazima uzae na mimi mtoto ambaye ndiye atakuja kuifanya kazimaalumu atakayo pangiwa na mkuu wa kuzimu ,”alisema kiumbe huyo.
“Nizae na wewe?”
“Ndiyo! Inatakiwa tufunge ndoa. Ndoa itafungwa kuzimu na atazaliwa mtoto mwenye nguvu ya ajabu sana,”
“Tokaaaaa! Tokaaaa,” nilipiga ukulele mkuu huku nikianza kumkabili kiumbe huyo.
Yule kiumbe alipiga ukelele na kubadilika ghafla. Akawa yule bibi kizee niliyekuwa nimekutana naye katika msitu wa Mputa kule shambani.
Akapandwa na ghadhabu kuu na akabaki akinitazama akiwa amesimama kwenye kona.
Baada ya hapo akapiga tena ukulele na kutoweka ndani humo kimuujiza.
*********
“Mamaaaa!” nikashituka kwa kupiga yowe kali kutoka usingizini huku ni kitweta sana.
Kwa haraka nilibaini haikuwa ndoto bali ni tukio la kweli lililotokea. Nikaanza kuvuta pumzi fupifupi huku mapigo ya moyo yakienda kasi.
Sikujua kama watoto au mke wangu walisikia kelele nilizo piga. Nikachukua kibatari na kungia chumbani.
Mke wangu alikuwa amelala fofo. Alikuwa amejifunika shuka jeupe siku hiyo. Baada ya kujiandaa kwaajili ya kulala nikapanda kitandani.
Kabla sijazima kibatari nikamgeuza mke wangu ili asogee upande wake. Nilipomgeuza nikapigwa na mshituko ghafla, baada ya kubaini aliyekuwa amelalla kitandani hapo hakuwa mke wangu bali ni yule Malaika wa kuzimu akiwa katika umbo lake la umalaika.. USIKOSE KUFUATILIA SEHEMU YA 5 YA RIWAYA HII YA KUSISIMUA