RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akishuhudia utiaji Saini Mkataba wa mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha kutoka Makutupora (Singida) hadi Tabora chenye urefu wa Kilometa 368 katika kipande cha tatu cha mradi huo (Lot III).
Wa kwanza (kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli nchini (TRC), Masanja Kadogosa, akiweka saini moja ya Kitabu cha Mkataba huo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Yapi Merkez ya Uturuki, Erdem Arioglu, katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam. (Picha na Ikulu)