Jeshi la Polisi Mkoani Tanga limefanikiwa kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa 35 ambao wamehukumiwa vifungo mbalimbali.
Kwa Mujibu taarifa iliyotolewa na Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Tanga Almachius Mchunguzi , watuhumiwa hao walikamatwa katika Kipindi cha mwezi mmoja.
Waliofikishwa Mahakamani na kuhukumiwa vifungo mbalimbali ni pamoja na watuhumiwa wa makosa ya kubaka ,kulawiti, na ukiukwaji wa sheria za usalama Barabarani ambapo watuhumiwa 20 walipatikana na hatia na kuhukumiwa vifungo magerezani.
Waliohukumiwa vifungo vya maisha jela ni Deogratius Alex (22),Samweli Ghamuga (25) wote kwa kosa la kubaka huku Athumani Rajab (19) amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kulawiti, Anthony Agustino na Twaha Rajabu wamehukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kubaka.
Watuhumiwa wengine ambao ni Omari- Mganga na Hussein Amiry ( 41) wamehukumiwa kifungo Cha miaka nane jela kwa kosa la wizi pamoja na Salimu Jumbe amehukumiwa miaka 27 jele kwa kosa la kuvunja nyumba na kuiba.
Kwa upande Wa makosa ya usalama Barabarani madereva wawili 02 wameondolewa madaraja kwenye leseni zao za dereva na 1 amefungiwa. Leseni ya udereva ambapo wengine wamelipa faini Mahakamani kwa makosa ya ukiukwaji washeria za usalama Barabarani.
Aidha Kamanda wa Polisi Amesema katika Kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Februari 21 Hadi machi 21 ,2024 Jeshi la Polisi Mkoa Wa Tanga limefanikiwa kukamata watuhumiwa 94 wakiwa na makosa mbalimbali ikiwemo makosa ya uvunjaji ,mauaji,kujeruhi ,kusafirisha wahamiaji haraku ,kujaribu Mali pamoja na kupatikana na silaha sita aina ya Gobole.
Kamanda huyo pia alieleza katika kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya wamefanikiwa kukamata wasafirishaji Wa dawa za kulevya aina yabmirungi na wauzaji Wa dawa za kulevya aina ya bhangi ambao ni Godwin Nemes (23) Mkulima Mkazi Wa Rombo Kilimanjaro akiwa na mwezake Christopher John (18) Mkulima Mkazi Wa Rombo ambapo kilo 307.5 za mirungu na kilogramu 73 za bhangi zimekamatwa.
Lakini pia katika hatua nyingine wamefanikiwa kukamata pikipiki 72 kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kutokuwa na namba za Usajili ,kutoboa Exos,kutokuwa na leseni nankutovaa kofia ngumu na wengine kujihusisha na vitendo vya kulihaligu.
Hata hivyo Kamanda huyo Amesema kuwa mara baada ya upelelezi kukamilika majalada yatapelekwa ofisi ya Taifa ya mashtaka kwa hatua zaid za kisheria.