Wednesday, May 21, 2025
English English Kiswahili Kiswahili
UMG
  • Mwanzo
  • UMG
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara
    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
    • All
    • Sports
    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

  • Michezo
    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • MAGAZETI
    • UELEKEO
  • UMG DIGITAL
  • UELEKEO DIGITAL
    • Instagram
    • Facebook
    • Twitter
    • Youtube
  • English English
  • Kiswahili Kiswahili

No Result
View All Result
UMG
No Result
View All Result
Mwanzo Habari Kitaifa

TANI 225 ZA MBEGU YA NGANO KUSAMBAZWA WILAYA TANO

admin by admin
March 15, 2021
in Habari Kitaifa
0 0
0
TANI 225 ZA MBEGU YA NGANO KUSAMBAZWA WILAYA TANO
0
SHARES
832
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Gift Mongi,  Monduli

BODI ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), imesema  inasambaza tani 225 za mbegu bora za ngano kwa wakulima wa wilaya tano kwenye mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

Aidha, bodi hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya kuzalisha na kusambaza mbegu ya Seed Co Tanzania, zimeahidi kutoa elimu na usaidizi wa kitaalamu kwa wakulima kwenye maeneo hayo ili kuwawezesha kupata mavuno mengi na bora.

Meneja wa CPB, Kanda ya Kaskazini, Hiza Kiluwasha, alikabidhi tani 17 za mbegu hizo kwa uongozi wa Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Ngano Monduli Juu (AMCOS), kwa lengo la kukuza uzalishaji wa zao hilo.

Mbegu hizo zilipokelewa na viongozi wa ushirika huo, akiwemo  Mwenyekiti, Moloimeti Sane na Katibu, Sifael Lormunyoi na kuhifadhiwa kwenye ghala la Kijiji cha Emairete, kilichoko Kata ya Monduli Juu, tayari kusambazwa kwa wakulima.

Imeelezwa kuwa mbegu hizo za ngano ya chakula, zina ubora wa hali ya juu kutokana na kuwa na protini ya kutosha, hivyo ngano itakayovunwa, inafaa zaidi kwa  matumizi ya nyumbani na viwandani, ambako hutumika kutengeneza mikate, keki, chapati na vyakula vingine.

“Tuna faraja kubwa sana kuletewa mbegu ya ngano na mbegu hii hatujawahi kuiotesha, hivyo tutajitahidi kuwa makini sana wakati wote wa kilimo cha ngano hii ya chakula, kuanzia ikiwa shamba mpaka kuvuna ili tuweze kujua ubora wake.

“Tunataka tufanye vizuri ili tuondokane na adha ya kilimo cha shayiri, ambacho tumedumu nacho kwa muda mrefu, lakini kwa sasa soko  linayumba,” alisema Sane.

Aliishukuru serikali kwa kuwasaidia kwenye zao la ngano ya chakula, ambalo lina bei ya uhakika kuliko mazao mengine wanayolima .

Katibu wa AMCOS, Lormunyoi alisema kitendo cha CPB, kuingia nao mkataba wa kununua ngano yote watakayoivuna, kimewapa faraja kwa kuwa wanalima wakiwa na uhakika wa kuuza mazao yao kwa bei nzuri.

Meneja wa CPB, Kanda ya Kaskazini, Kiluwasha, alisema ngano hiyo imesambazwa kwenye maeneo, ambayo wameishaingia mikataba na wakulima kwa ajili ya kununua ngano yao pindi wakivuna.

Alisema hilo linatekelezwa kanda ya kaskazini, ambako tayari wameshakabidhi mbegu hizo za ngano kwa wakulima wa Nangwa, Wilaya ya Babati, mkoani Manyara, Karatu na Monduli Juu, mkoani Arusha na West Kilimanjaro, Wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro.

“Tutahakikisha wakulima tulioingia nao mkataba wote wanapata mbegu na Jumatatu (leo), wote watakuwa wanapanda mbegu hizo shamba. Hii ngano ni ile yenye ubora, imekidhi viwango, itaanza kupandwa Jumatatu. Tunatekeleza maagizo ya Rais Dk. John Magufuli, kuhakikisha zao la ngano linafufuliwa na tunahamasisha wakulima wengi kulima,” alisema.

Alisema CPB imeingia makubaliano ya kimkataba  na wakulima  wa Monduli Juu, kuhakikisha wanapolima, wanawapatia mbegu na wanapovuna wananunua ngano yao yote.

Kiluwasha, alisema wameshirikiana na Kampuni ya Mbegu ya  Seed Co Tanzania,  kuagiza mbegu hizo zinazozalishwa na kampuni hiyo nchini Zambia, ambazo wanawauzia wakulima kwa sh. 2,900, kwa kilo moja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Seed.Co, ukanda wa Afrika Mashariki, Clive Mugadza, alisema kampuni yake italeta wataalamu wake wawili watakaopita kwenye maeneo ya mashamba ya wakulima waliouziwa mbegu hizo ili kuwapatia elimu na ujuzi zaidi juu ya namna bora ya kulima ngano hiyo, ili iwe na matokeo mazuri.

Aliwashukuru CPB na serikali kwa kuiamini kampuni yao na kufanya kazi pamoja huku akisifu namna taasisi nyingine za serikali zinazohusika na kuangalia ubora, likiwemo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), kwa kazi waliyoifanya na kuhakikisha mbegu zinawafikia wakulima kwa wakati.

admin

admin

Stay Connected test

  • 139 Follower
  • 204k Subscriber
  • 23.9k Follower
  • 99 Subscriber
  • Trending
  • Comments
  • Latest
MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

July 9, 2021
BREAKING NEWS: RATIBA LIGI KUU NBC MSIMU WA 2023/2024 HII HAPA

BREAKING NEWS: RATIBA LIGI KUU NBC MSIMU WA 2023/2024 HII HAPA

August 7, 2023
TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

July 9, 2021
BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

August 9, 2021
NDUGU MATATANI KUMSHAMBULIA, KUMJERUHI MWENZAO KISA NG’OMBE

NDUGU MATATANI KUMSHAMBULIA, KUMJERUHI MWENZAO KISA NG’OMBE

0
WAHANDISI WA HALMASHAURI WAMEKUA WAKIIKOSEA SERIKALI KWAKUTOA TAARIFA ZA UONGO

WAHANDISI WA HALMASHAURI WAMEKUA WAKIIKOSEA SERIKALI KWAKUTOA TAARIFA ZA UONGO

0

OFISA ELIMU, MHANDISI, MKUU WA SHULE WAKALIA ‘KUTI KAVU’

0
STENDI YA ZAMANI UBUNGO  KUJENGWA DEPO MABASI MWENDOKASI

STENDI YA ZAMANI UBUNGO KUJENGWA DEPO MABASI MWENDOKASI

0
TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

November 20, 2024

YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 12, 2024

November 12, 2024
YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 11, 2024

YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 11, 2024

November 11, 2024
YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 1, 2024

YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 1, 2024

October 31, 2024

Recent News

Instagram Youtube Twitter Facebook

We are a diverse team of experts, innovative thinkers, creative designers, writers, innovators, strategists, pyschologists, comunictaors and web developers. UMG is extremely passionate about growing clients’ businesses, helping them achieve their goals and making a difference by raising the creative and communications industry standards in Tanzania.

Follow Us

Browse by Category

  • Afya Makala
  • BIASHARA
  • BURUDANI
  • Business
  • HABARI KIMATAIFA
  • Habari Kitaifa
  • Habari Picha
  • KIMATAIFA
  • MAGAZETI
  • MAHAKAMANI
  • MAKALA
  • MAKALA AFYA
  • MAKALA-BURUDANI
  • MICHEZO
  • MICHEZO KIMATAIFA
  • MICHEZO KITAIFA
  • MICHEZO-MAKALA
  • MICHEZO-MASUMBWI
  • MITINDO
  • RIWAYA
  • SIASA
  • Sports
  • Uncategorized

Recent News

TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

November 20, 2024

YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 12, 2024

November 12, 2024

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

No Result
View All Result

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In