Na MWANDISHI WETU
MWANAMUZIKI Rajabu Kahali ‘Harmonize’ amesema kuwa huenda mwaka huu akatoa nyimbo zitakazofanya vizuri zaidi sokoni kwa kuwa muda wote ana furaha.
Akizungumza katika kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam jana, Harmonize alisema anapokuwa na furaha hufanya kazi nzuri kuliko wakati mwingine wowote.
Harmonize alisema furaha aliyonayo sasa ni kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamke anayemuelewa na kumshauri vitu vya kufanya ambavyo vinamuingizia kipato kikubwa.
Alipoambiwa amtaje mpenzi wake, Hamonize alisema ‘Kwani hamjui kuwa mimi na Kajala Masanja ni wapenzi?.
Alisema licha ya mashabiki na watu wengine kwenye jamii kudhani kuwa uhusiano wake na Kajala ni wa kuigiza anataka kuwathibitishia kuwa wana uhusiano wa kweli na ni mwanamke anayempenda kwa dhati.
“Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kunipa mwanamke mwenye akili na anayependa maendeleo, nina amani na furaha tele na hata ninapokaa kuandaa kazi zangu muda mwingi natabasamu huku nikiamini hata kazi ninayoifanya itakuwa bora,” aliongeza.
Harmonize na Kajala ambaye ni msanii wa filamu walionekana kwa mara ya kwanza hadharani Februali mwaka huu kabla ya kuthibitisha kuwa na uhusiano.
Kajala amewahi kutamba katika filamu ya Kigodoro, ‘Jeraha la Moyo’, ‘House Boy’, ‘Vita Baridi’, ‘House Girl & Boy’.
Nyingine ni ‘Dhuluma’, ‘Shortcut’, ‘Basilisa’, ‘You Me and Him’ na ‘Devils Kingdom’.