Na Mwandishi Wetu
KUFUATIA kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, aliyefariki Dunia katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es salaam, Spika wa Bunge, Job Ndugai, ameziagiza Kamati zote za Kudumu za Bunge zilizokuwa Mikoani kwenye ziara kurejea mara moja jijini Dodoma.
Spika wa Bunge katika Salamu zake za rambirambi kwa watanzania amesema Taifa limepoteza Kiongozi mahiri na Shujaa aliyewapigania wanyonge, Taifa litaendelea kumkumbuka.