Na Mwandishi Wetu
WAKILI wa Kujitegemea, Sylvester Sebastian, ametolea ufafanuzi kuhusu mkanganyiko wa muda wa kuapishwa kwa Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iwapo Rais aliyepo madarakani atafariki Dunia, akisema Makamu wa Rais atapaswa kuapishwa kuwa Rais ndani ya siku Saba.
Akizungumza na #UhuruFM, Wakili Sebastian, amesema japo Katiba haijawekwa wazi, lakini utaratibu wa kawaida ambao upo katika Katiba kifungu cha 42, kinasema endapo Rais ametangazwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, isizidi siku Saba awe ameapishwa.
Makamu wa Rais, mwenye umri wa miaka 61, atahudumu katika wadhfa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha miaka Mitano ambacho Magufuli alikianza baada ya kushinda muhula wa Pili.
Mama Samia atakuwa Rais wa Kwanza na wa pekee Mwanamke Afrika Mashariki.