UMOJA wa Falme za Kiarabu (UAE), unakusudia kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,kuboresha utoaji wa huduma za afya na masuala mengine yanayohusu maendeleo ya jamii visiwani humo.
Nia hiyo imebainika leo, baada ya maofisa wa Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii UAE, kufanya ziara rasmi katika hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja, Unguja na kutembelea shule (skuli) ya Mtopepo.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Dk. Omar Dadi Shajak, aliongoza ujumbe huo wa wageni, sambamba na Balozi wa Umoja wa UAE hapa nchini, Khalifa Almarzouqi.
Na Thabit Madai



























