DIWANI wa Kata ya Kivukoni, Dar es Salaam, Sharik Choughle, amefanya ziara katika banda la maonyesho la Kampuni ya Uhuru Media Group (UMGL), wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo, Radio Uhuru FM na Uhuru Online, katika viwanja vya Sabasaba.
Akiwa katika banda hilo, diwani huyo amepongeza jitihada zinazofanywa na uongozi wa UMGL kuvisimamia vyombo hivyo ambavyo ni mali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Diwani Sharik amesema, amekuwa mdau wa muda mrefu wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na msikilizaji mzuri wa redio Uhuru FM na kwamba anaridhishwa na weledi wa wafanyakazi katika utekelezaji wamajukumu yao na ubora wa maudhui ya vyombo hivyo.
“Mko vizuri, nimewafuatilia kwa muda mrefu na sasa nimeona mmegeukia pia uchapaji maudhui mtandaoni kwa kupitia Uhuru Online, nawapongeza sana, ongezeni uwekezaji kwenye mambo muhimu kama vifaa na mengine, mtakuwa vizuri zaidi,” amesema.



























