MBUNGE wa Lindi Mjini, Hamida Abdallah, amewataka vijana Mkoani Lindi, kuwa wabunifu mahali walipo, ili wajiajiri na kuondokana na umasikini badala ya kukaa bila kazi.
Mbunge huyo ametoa kauli hiyo akifungua Baraza la Vijana la Manispaa ya Lindi, ambapo akiwasihi kuwa na ushirikiano na upendo katika safari hiyo ya mafanikio na maendeleo kimaisha.
Hamida amesema ni jambo la msingi kwa vijana kujiunga na mafunzo ya ufundi katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali, ikiwemo VETA ambacho serikali inakingalia kwa jicho la kipekee.
“Nawapenda sana vijana wangu wa Manispaa ya Lindi, niwaombe mfanye kazi kwa juhudi zote na mnajua Rais Mama Samia Suluhu Hassan, anawapenda sana vijana na ndio maana katika uongozi mbalimbali wa taifa letu, vijana mnaongoza kuwekwa katika nyadhifa mbalimbali,” amesema mbunge huyo.
Na Sophia Nyalusi