WAZIRI wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda, amewataka wakulima kuzingatia zaidi zao la kahawa kwa kuwa linaleta tija na kuongeza uchumi wa nchi.
Akizungumza hivi karibuni katika maonyesho ya 45 ya Sabasaba, alisema hivi sasa Serikali inahimiza kilimo cha mazao ya yakiwemo Kahawa, Pamba, Korosho, Tumbaku, Zabibu na mengine.
“Hivi sasa tumejikita zaidi kuhimiza kilimo cha mazao ya mkakati ili kiweze kuleta tija na kuongeza uchumi wa nchi”,amesema Profesa Mkenda .
Amesema hata Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza zaidi kilimo chenye kuleta tija na kuongeza maeneo kwa ajili ya kilimo.
Akitolea mfano kuongeza tija ya mazao alisema takwimu ya kahawa ya arabika msimu wa mwaka 2020/21thamani ya fedha imeongezeka .
“Ukiangalia takwimu Kahawa yetu ya Arabika msimu wa 2020/21 tumepata Dola milioni 82 tumepata kwa sababu tija yetu ipo chini ambako kwa mti mmoja ni gram 300 hadi 350 tukienda kwenye kilogram 11 hadi kilogram 1.5 kwa maeneo haya haya tunayolima tungeongeza kipatochetu cha fedha za kigeni kutoka Dola milioni 82 na kuongeza kiasi cha mil. 47.amesema.
Ameongeza, “si suala la kusema kuongeza sehemu ya kulima bali muhimu ni kuongeza uzalishaji sehemu tunayolima”,amesema
Na MWANDISHI WETU



























