BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Twaha Kassim ‘Twaha Kiduku’, amewaomba wadau na wapenzi wa ndondi kujitokeza kwa wingi katika pambano lake dhidi ya Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’.
Pambano hilo linalokwenda kwa jina la ‘Face Off’, litafanyika Agosti 14, mwaka huu katika Uwanja wa Florida mkoani Morogoro, pia Agosti 20 mwaka huu watakutana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa ubungo Plaza.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka kambini, Kiduku, amesema bado anaendelea kujifua ili siku ya pambano ampasue mpinzani wake.
“Nashukuru Mungu mashabiki zangu na wakazi wa Morogoro kwa kuendelea kunipa sapoti.
Ngumi ni kazi yangu ambayo inasimamia maisha yangu, hivyo wajibu kuongeza bidii katika mazoezi yangu na nawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi,” alisema.
Katika pambanio lilopita, Kiduku alimpiga Dullah Mbabe kwa pointi katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, mwaka jana.
Na AMINA KASHEBA