RAIS Samia Suluhu Hassan, amemteua Dk. Stergomena Tax, kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Spika Job Ndugai, tayari amemwapisha kabla ya shughuli zingine za Bunge kuendelea.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusaini na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu, Dk. Stergomena ameteuliwa kutoka katika nafasi 10 za wabunge wa kuteuliwa na Rais.
Kabla ya uteuzi huo, Dk. Stergomena alikuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye amemaliza muda wake Agosti, mwaka huu.



























