SHINDANO la kutafuta mlibwende ukanda wa pwani (Miss Easter zone) linatarajia kufanyika Septemba 24 mwaka huu katika ukumbi wa Daynastic beach Ununio, Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi Wahabari jijini Dar es Salaam Mratibu wa shindano hilo, Nancy Matta amesema Mshindi wa kwanza wa Kinyang’anyiro hicho atajinyakulia kitita cha shilingi milioni tatu, huku wapili akipatiwa shilingi milioni mbili na nusu na kwa Mshindi wa tatu Shilingi milioni moja.
Nancy ameeleza kwa namna Shindano Hilo limeweza kupata washiriki kupitia Mikoa ya pwani ipatayo minne.
Hata hivyo amefafanua kuwa Kutokana na nafasi yake na uzoefu wake katika Mashindano hayo anaamino kuwa Shindano Hilo itakua ni sehemu ya washiriki kupata tiketi ya kushiriki Mashindano ya Miss Tanzania mwaka huu.
“Shindano limeshirikisha mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara na Pwani ambao washindi watapata nafasi ya kushiriki mashindano ya Miss Tanzania na kuwakilisha taifa katika shindano la dunia, ‘ amesema.
Mratibu huyo ameongezea Kuwa Septemba 22 mwaka huu kutafanyika shindano la kumtafuta warembo wenye vipaji’ Miss Talent’.
“Shindano hili litafanyika mkoani Morogoro,nawaomba wadau wa urembo kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia vipaji lukuki kwa warembo hawa.” amesema.
Ofisa Habari wa bodi ya Utalii, Maria Mafie amesema shindano hilo litasaidia kukuza na kuendeleza utalii wa ndani.
Maria amefafanua kuwa ugonjwa wa corona umesababisha kupungua kwa watalii nchini, hivyo shindano hilo litasaidia kuhamasisha watanzania kujitokeza katika vivutio.
Na AMINA KASHEBA