BARAZA la taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), linatarajia kuzindua Kanzi data ya wafanyabiashara wa Tanzania ili kuongeza wigo wa uwekezaji.
Katibu Mtendaji wa baraza hilo Beng’i Issa ameeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu wakati Kongamano la 5 la mwaka la uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Amesema kupitia kanzi data hiyo itasaidia wafanyabiashara na makampuni ya ndani kujulikana kimataifa hali itakayosaidia kukuza uwekezaji.
Pia, amesema kupitia kongamano hilo watapata nafasi ya kupima utekelezaji wa sera ya uwekezaji wananchi kiuchumi pamoja na shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kongamano hilo Suleiman Malela amesema kuwa kongamano hilo ni muhimu kwa kuwa litawaweza kuwakutanisha wadau mbalimbali na kufungua fursa zitakazoleta maendeleo.
Kongamano la 5 la Kitaifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi linatarajiwa kifanyika Jijini Dodoma October 4 mwaka huu ambapo mgeni rasmi atakuwa ni waziri mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Kassimu Majaliwa .



























