WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu, ametoa wito kwa wakurugenzi wa Halmashauri kutotumia nafasi zao kudhalilisha watumishi wakike waliopo kwenye nafasi za chini kisa wamewakataa kimahusiano.
Amesema hatamvumilia mkurugenzi wa aina hiyo kwa sababu ni uonevu udhalilishaji kisa tuu anatumia cheo na wadhifa alionao hivyo kusababisha watumishi wengine wa kike kupigana.
“Nimepata kesi za aina hii unakuta kuna mtumishi wa kike amemkataa mkurugenzi sasa kwa kumkomesha anaamua kutomruhusu kwenda kwenye semina hii siyo tabia nzuri, kwa upande wa wakurugenzi wanawake sijapata kesi za aina hii.
“nawasihi kalindeni utu na heshima mliyopewa na Rais Samia Suluhu Hassan angalieni watu mnaotoka nao maana sikatazi mtu kuwa na mahusiano lakini kuna baadhi ya wakurugenzi kila mfanyakazi mzuri ni wake,”amesema.
Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati wa kikao kazi cha siku mbili na wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Na SELINA MATHEW, Dodoma



























