MFANYABIASHARA na Muwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohamed Dewji, ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Klabu hiyo.
Amesema nafasi hiyo itachukuliwa na aliyekuwa Makamu wake Salim Abdallah (Try Again).
Bilionea MO amefikia uamuzi huo kutokana na safari za nje ya nchi hivyo mara nyingi kutokuwa nchini.
“Mmetuunga mkono kwa miaka minne ya Uongozi wangu kama Mwenyekiti wa Bodi, kwenye miaka minne tumepata mafanikio makubwa tumeshinda Ligi mara 4 na kufanya vizuri kwenye ‘Champions League’ muda umefika kama Mohammed na tumekubaliana mimi nitajiuzulu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC naomba sana msifikie kuwa Mimi nimeondoka Simba bali bado ni Muwekezaji,”amesema.