WANANCHI 20,550 wa Halimashauri za Mkoa wa Mara wamejitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19, tangu Serikali ianze kutoa huduma hiyo kwa wananchi kwa lengo la kujikinga na maambukizi ya virusi vya UVIKO-19.
Mganga Mkuu Hospitali ya Mkoa wa Mara, Juma Mfanga amesema serikali kupitia wataalam wa Afya wamefanikiwa kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali hali iliyopelekea wananchi kuendelea kuhamasika kupata chanjo ya Uviko-19.
Amesema awali mkoa wa Mara ulipokea chanjo 25,000 ambazo zote zimetumika baada ya wananchi kuhamasika hali iliyopelekea kuomba msaada wa chanjo ya Uviko-19 katika mkoa wa Mwanza ili kuendelea kutoa huduma hiyo kwa wananchi.
Katika hatua nyingine Dr Mfanga amesema wataalam wa Afya tayari wameanza kutoa huduma hiyo katika maeneo ya makazi na sehemu zenye mikusanyiko na sehemu za magulio ili kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi na hivyo kuwafikia wananchi 900,000 wa mkoa huo.
Mmoja ya mkazi wa manispaa ya Mkendo Manispaa ya Musoma, amesema serikali inatakiwa kuendelea kutoa elimu kupitia kampeni mpya ya uhamasishaji ili wananchi waweze kufikiwa na wataalam wa afya waweze kujibu hoja zao.
Na Emmanuel Chibasa-Mara