MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Arusha, Hezron Mbise ametoa viti Mia Moja kwa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Monduli ili kujikwamua kiuchumi.
Mbise ametoa viti hivyo wakati ziara yake ya kikazi wilayani ya kukagua uhai wa Jumuiya hiyo, Miradi ya Jumuiya pamoja na Utekelezaji wa Ilani CCM.
“Viti hivi ni kwa ajili ya kukodisha,Naomba mvitunze ili viwasaidie kupata fedha za kuendesha vikao vya Jumuiya badala ya kwenda kuomba msaada”.
Pia mwenyekiti huyo amepokea wanachama wapya wa Jumuiya 240 kutoka wilaya ya Monduli.