RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi, Évariste Ndayishimiye, baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, kwa ziara ya kikazi ya siku 3.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi, Évariste Ndayishimiye, wakati nyimbo za Mataifa mawili Tanzania na Burundi pamoja na wimbo wa Afrika Mashariki zikipigwa baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akimtambulisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi, Évariste Ndayishimiye kwa Viongozi mbalimbali wa Serikali baada kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
RAIS wa Jamhuri ya Burundi, Evariste Ndayishimiye akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi, Evareste Ndayishimiye Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo Rasmi na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi, Evariste Ndayishimiye, aliyekuwa akiongoza ujumbe kutoka Burundi katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma