MICHEZO: KOCHA wa #SIMBASC Didier Gomes, amebwaga manyanga katika Klabu hiyo kwa kuomba kuchana na Simba kuanzia leo Oktoba 26, 2021.
Taarifa kutoka Simba SC imethibitisha kupokea ombi hilo na kumtangaza aliyekuwa kocha Msaidizi Thierry Hitimana kuwa Kocha Mkuu katika kipindi cha mpito akisaidiwa na Selemani Matola.