MABONDIA zaidi ya 30 leo wamepima uzito na afya kuelekea katika pambano la ‘Dar Boxing Derby’ zoezi hilo lilifanyika katika uwanja wa Dar es Kinesi uliopo Urafiki, Dar es Salaam.
Pambano hilo litafanyika kesho katika Uwanja wa Kinesi uliopo Urafiki, Dar es Salaam.
Akizungumza na UhuruOnline, muandaaji wa pambano hilo, Kapteni Selemani Semunyu, amesema maandalizi yamekamilika, sasa wanasubiliwa mabondia kupima ili kuonyesha burudani kwa watanzania.
“Maandalizi yamekamilika leo mabondia wamepima uzito ili kuthibitisha kama kesho watacheza katika pambano la ‘Dar Boxing Derby Mwana Ukome,” amesema Semunyu.
Muandaaji huyo ametoa wito kwa wadau wa ndondi kujitokeza kwa wingi katika pambano hilo ili kushuhudia mtanange mkali kati ya Mabibo na Manzese.
“Hii inaitwa vita ya Wilaya hapa kuna Fransic Miyeyusho kutoka Kinondoni akizichapa na Adam Kipenga kutoka Manzese, lakini kuna Idd Pialari akuchuana na Ramadhani Shauri kutoka Mabibo hii ni Derby ya kweli,” Semunyu.
Semunyu ametaja mabondia wengine wanaozichapa ni Selemani Kidunda dhidi ya Jacob Maganga ambao watagombania mkanda wa Ubingwa wa Taifa, Grace Mwakamele atacheza na Asha Ndegele, Hassan Ndonga kuzichapa na James Kazibange na George Bonabucha atamenyana na Haji Juma.
Fransic amewataka wadau na wapenzi wa masumbwi kujitokeza katika pambano hilo ili kushuhudia burudani kutoka kwake.
“Nawaomba watanzania wote wajitokeza katika uwanja wa Kinesi kuja kushuhudia ninamvyomchakaza mtu,” amesema Fransic
Bondia, Ramadhani Shauri amesema amejipanga vizuri ili kuonesha mchezo mzuri na kupata ushindi katika pambano hilo.
Shauri ameeleza kuwa atahakikisha anamchakaza mpinzani wake, Idd Pialari katika pambano hilo.
Na AMINA KASHEBA