Sunday, March 15, 2026
27 °c
Dar es Salaam
25 ° Thu
25 ° Fri
25 ° Sat
25 ° Sun
25 ° Mon
English English Kiswahili Kiswahili
UMG
  • Mwanzo
  • UMG
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara
    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
    • All
    • Sports
    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

  • Michezo
    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • MAGAZETI
    • UELEKEO
  • UMG DIGITAL
  • UELEKEO DIGITAL
    • Instagram
    • Facebook
    • Twitter
    • Youtube
  • English English
  • Kiswahili Kiswahili
  • Mwanzo
  • UMG
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara
    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
    • All
    • Sports
    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

  • Michezo
    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
No Result
View All Result
UMG
No Result
View All Result
Mwanzo Habari Kitaifa

MAADHIMISHO 60 YA UHURU YAMEFANA

admin by admin
December 10, 2021
in Habari Kitaifa
0 0
0
MAADHIMISHO 60 YA UHURU YAMEFANA

AMIRI JESHI Mkuu, Rais Samia Suluhu Hassan, akiwasili Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, kuongoza maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo

0
SHARES
224
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

MAADHIMISHO ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, yamefana jijini Dar es Salaam yakipambwa na vikosi vya gwaride na halaiki maalumu kutoka kwa watoto wa  shule za msingi.

Aidha, maadhimisho hayo, yalikuwa ya aina yake katika Uwanja wa Uhuru ambao unaokadiriwa kuingia watu 23,000, uliokuwa umefurika  na baadhi ya wananchi kulazimika kukaa Uwanja wa Mkapa.

Sherehe za maadhimisho hayo, zilianza saa 2:00 asubuhi huku kukiwa na utulivu ambapo onyesho la uokoaji lilifanywa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na kufuatiwa na kwata ya Jeshi la Polisi kabla ya uhuru, waliovalia kaptura nyeupe, soksi ndefu nyeupe na kofia nyekundu.

Walipita kwa mwendo wa ukakamavu na haraka kuzunguka uwanja kuonyesha namna Jeshi la Polisi lilivyokuwa kabla ya uhuru huku mikononi wakishika fimbo

Wakati kwata inaendelea Rais mstaafu wa  Malawi, Dk. Joyce Banda aliwasili uwanjani hapo saa 2:38 asubuhi huku wageni wengine waalikwa, viongozi wa serikali na wananchi wakiendelea kuwasili.

Saa 2:46 Rais wa Mahakama ya Afrika aliwasili huku gwaride la kimya kimya lililofanywa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likionyesha umahiri na maumbo mbalimbali ikiwemo nyota na namba 60 kuashiria maadhimisho hayo.

Baadaye Makamu wa Rais wa Msumbiji aliwasili na kisha Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na mwenza wake waliwasili saa 2:52.

Kwata ya kimyakimya ilipokamilika wasanii mbalimbali walipata fursa ya kutumbuiza katika sherehe hizo, wakitanguliwa na Bendi ya TOT.

Saa 3:03 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah na mwenza wake waliwasili na kufuatiwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete, kisha Naibu Waziri Mkuu wa Eswatini na mwenza wake waliowasili saa 3:07.

Dakika nane baadaye Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Kitaifa aliwasili uwanjani hapo akiwa na mwenza wake kisha kufuatiwa na Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Banzumbanja, aliyewasili saa 3:16.

Alifuata ni mjane wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, mama Maria Nyerere aliyewasili saa 3:20 na kufuatiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, mwenza wake na Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi waliowasili saa 3:25.

Sherehe hizo zilizopambwa kwa nakshi za mabango yaliyoandikwa ‘MIAKA 60 YA UHURU Tanzania Imara, Kazi Iendelee’ ikiwa ndiyo kauli mbiu ya sherehe hizo, zilihudhuriwa na wajane wa waasisi wa taifa ambao ni Mama Maria Nyerere na Mama Karume wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Viongozi waliendelea kuwasili ambapo saa 3:30 Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango aliwasili na mwenza wake, kisha tarumbeta kupigwa kuashiria gwaride kuingizwa uwanjani.

Wakati gwaride linaendelea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) aliwasili saa 3:33 na kisha gwaride kuanza kuingia uwanjani.

Kuingia kwa gwaride kuliamsha hisia za wananchi wengi uwanjani hapo ambapo waliibua shangwe, nderemo na vifijo huku vikosi vya majeshi vilivyojigawa kwa makundi 13 vikiingia kutoka pande zote za uwanja kwa mpangilio maalumu wakionyesha mwendo wa madaha na ukakamavu huku kila kikosi kikiwa kimevalia sare zake.

Aidha,  kikosi cha bendera chenye askari watano kiliingia uwanjani na hivyo wananchi na askari kusimama kutoa heshima, huku ushiriki wa Jeshi la Uhamiaji ambalo ni mara ya kwanza kuwa katika  gwaride na maonyesho hayo kwa ujumla ikiwa ni kivutio.

Saa 3:53 mwenza wa Rais wa Tanzania, Hafidh Ameir, aliwasili kwa gari aina ya BMW na kufuatiwa na Rais wa Visiwa vya Comoro, Azali Ousumane aliyeingia uwanjani hapo  saa 3:55.

Msafara wa mwenza wa Rais Samia, ulifungua kuwasili kwa wakuu wa nchi ambapo Rais wa Msumbiji, Felipe Nyusi, aliwasili saa 3:56.

Mnamo saa 3:57 aliwasili Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na saa 4:01 aliwasili Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambapo wananchi waliibua shangwe na vigelegele wakimshangilia.

Rais Samia, aliwasili uwanjani hapo saa 4:18 akiwa amebebwa katika gari maalumu la wazi na kuzungushwa uwanjani kwa dakika nne huku akisalimia kwa kupungia wananchi mkono katika kila upande.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akipokea Heshima ya Wimbo wa Taifa katika Maadhimisho ya kutimia miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika, Desemba 09, 2021 katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Shangwe ziliibuka katika kila jukwaa alilokaribia uwanjani hapo, huku akionekana nadhifu akiwa amevalia mtandio mwekundu na suti nyeusi na kama ilivyo kawaida yake akitoa tabasamu kuashiria kufurahishwa na sherehe hizo.

Aliposhuka alikwenda katika jukwaa maalumu saa 4:23 kuruhusu wimbo wa taifa kupigwa na wimbo wa Afrika Mashariki huku mizinga 21 ikipigwa.

Saa 4:27 Rais Samia alianza kukagua gwaride kwa mwendo wa ukakamavu akisindikizwa na wimbo wa ‘Tanzania Tanzania’ kitendo kilichofanyika kwa dakika 10 na kisha akapanda jukwaa kuu kuungana na viongozi wenzake.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika Maadhimisho ya kutimia miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika Desemba 09, 2021 katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Saa 4:38 gwaride lilianza kuchezwa kwa mwendo wa polepole kuzunguka uwanja likionyesha ukakamavu na umahiri likisindikizwa na Brass Band ya JWTZ  na kisha mwendo wa haraka.

Madaha ya majeshi hayo katika kuchezea silaha wakati wa  gwaride, ndilo jambo lilioonekana kukonga nyoyo za wengi waliohudhuria sherehe hizo kwani wakati wote walipiga makofi na kushangilia.

Gwaride hilo lilifanyika kwa dakika 50 na kisha saa 5:18 askari kikosi cha wanamaji waliobeba mizigo yenye uzito wa kilo 30 walipita na kutoa heshima kwa Rais huku wakiwa wamevalia sare nyeusi.

Baada ya kikosi hicho, wengine waliopita ni askari wa wana maji waliobeba mabegi yenye uzito wa kilo 50 ndani yakiwa na vitu vya kuwasaidia kuishi kwa siku kadhaa wanapokuwa vitani.

Saa 5:27, gwaride lilimalizika na kutoka uwanjani ili kuruhusu ratiba nyingine ziendelee.

Aidha saa 5:35, watoto wa halaiki walionekana kuwa kivutio zaidi katika sherehe hizo kwa kuonyesha matukio ya kutengeneza maumbo ikiwemo ya miaka 60 ya Uhuru, kusisitiza uimara wa Jeshi la Tanzania na umuhimu wa afya njema kwa taifa.

VIJANA wa halaiki wakionyseaha ukakamavu mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam Desemba 9, 2021.

Pia, walionyesha matukio ya  kudhibiti moto, jinsi ya kutumia silaha wakiwa vitani, namna waasisi ya taifa walivyojitoa katika kupigania Uhuru  na michezo mbalimbali.

Watoto hao walitumia fursa hiyo, kutoa salamu na ujumbe uliosisitiza miaka 60 ya Uhuru Tanzania Imara Kazi Iendelee na kuimba wimbo maalumu ukieleza kuwa ni furaha kwa kila mtanzania kuzaliwa katika taifa hili lenye utamaduni, umoja na mshikamano.

Saa 6:51, yalianza maonyesho ya askari wakiwa wamevalia mavazi ya vikosi vya zamani kabla ya uhuru, yaliyofanywa na JWTZ.

Askari hao walivalia mavazi ya kaptura zenye rangi ya kaki na kofia huku wakiwa pekupeku, mavazi yaliyovaliwa miaka ya nyuma kabla ya uhuru.

Pia walionyesha mavazi ya Jeshi la Ulinzi kwa sasa, Jeshi la akiba na vijana wa skauti.

Awali, jeshi lilionyesha namna watumishi wake wanavyoweza kubeba mizigo ya kuanzia kilo 30, 50 na 100 wakiwa vitani na silaha ambao walipita mbele ya umati wa watu katika sherehe hizo.

VIKOSI mbalimbali vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ vikipita Kikakamavu mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan, katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, 9 Desemba, 2021.

Saa 7:00 zilipita ndege mbili kwa ajili ya usafirishaji aina ya helikopta huku onyesho la silaha, zana za kivita likiendelea mbele ya Rais na wakuu wengine wa nchi za Afrika waliohudhuria sherehe hizo.

Wakati huo ndege nyingine ya usafirishaji wa vifaa mbalimbali vya kijeshi na kutoa msaada wa kiraia ilipita.

Miongoni mwa silaha hizo zilikuwepo zinazompiga adui aliyejichimbia katika handaki, kombora la kuharibu ngome ya silaha za adui, vifaru, mizinga inayotumika kupiga adui wa wazi.

Onyesho lililowaduwaza wengi ni kifaru chenye uwezo wa kupita katika maji na nchi kavu ambacho hutumiwa na jeshi la wana maji.

Pia,  jeshi lilitumia maonyesho hayo kuonyesha daraja lenye uwezo wa kujengwa na kutenguliwa kwa muda wa dakika 20 na jingine dakika 60.

Kadhalika zilionyeshwa silaha za kutungulia ndege za adui inayopita kimo cha chini huku ndege tatu za mafunzo ya kivita zikipita.

Pia, kilionyeswa kikundi cha mbwa vita ambao kazi yao ni kukamata na kushambulia maadui, kutegua mabomu na kusaka zilipo silaha za adui.


Saa 7:15 zilipita ndege vita tatu zikiwa katika mwendo kasi, baadaye ndege moja ilipita kwa kasi zaidi, nyingine mwendo wa kujiviringisha na ya mwisho ilipita ikitoa heshima kwa Rais.

Saa 7:29 macho  yaligeukia kaskazini mwa uwanja ilipokuwa inatokea helikopta ya uokoaji ya JWTZ, ambazo zilishusha askari kwa kamba na kuonyesha namna wanavyoweza kutua kwa kasi  na kunyakuliwa kwa kamba huku wakipepea bendera ya taifa tukio lililoamsha furaha kwa wananchi wakionyesha kuridhishwa na namna jeshi lilivyojidhatiti katika ulinzi na usalama.

MARIAM MZIWANDA NA JUMA IS’HAKA

admin

admin

Stay Connected test

  • 138 Follower
  • 205k Subscriber
  • 23.9k Follower
  • 99 Subscriber
  • Trending
  • Comments
  • Latest
MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

July 9, 2021
BREAKING NEWS: RATIBA LIGI KUU NBC MSIMU WA 2023/2024 HII HAPA

BREAKING NEWS: RATIBA LIGI KUU NBC MSIMU WA 2023/2024 HII HAPA

August 7, 2023
TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

July 9, 2021
BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

August 9, 2021
NDUGU MATATANI KUMSHAMBULIA, KUMJERUHI MWENZAO KISA NG’OMBE

NDUGU MATATANI KUMSHAMBULIA, KUMJERUHI MWENZAO KISA NG’OMBE

0
WAHANDISI WA HALMASHAURI WAMEKUA WAKIIKOSEA SERIKALI KWAKUTOA TAARIFA ZA UONGO

WAHANDISI WA HALMASHAURI WAMEKUA WAKIIKOSEA SERIKALI KWAKUTOA TAARIFA ZA UONGO

0

OFISA ELIMU, MHANDISI, MKUU WA SHULE WAKALIA ‘KUTI KAVU’

0
STENDI YA ZAMANI UBUNGO  KUJENGWA DEPO MABASI MWENDOKASI

STENDI YA ZAMANI UBUNGO KUJENGWA DEPO MABASI MWENDOKASI

0

Découvrez le Frisson des Jeux Crash d’AviaMasters

March 15, 2026

ChachaBet Official Speel & Claim 225% Bonus + Free Spins

March 15, 2026

Avanafil og Dapoxetin: Hvordan skal det indtages?

March 15, 2026

Woopwin Casino Online Casino Bonus & Gratis Spins Review 2026

March 15, 2026

Recent News

Découvrez le Frisson des Jeux Crash d’AviaMasters

March 15, 2026

ChachaBet Official Speel & Claim 225% Bonus + Free Spins

March 15, 2026

Avanafil og Dapoxetin: Hvordan skal det indtages?

March 15, 2026

Woopwin Casino Online Casino Bonus & Gratis Spins Review 2026

March 15, 2026
Instagram Youtube Twitter Facebook

We are a diverse team of experts, innovative thinkers, creative designers, writers, innovators, strategists, pyschologists, comunictaors and web developers. UMG is extremely passionate about growing clients’ businesses, helping them achieve their goals and making a difference by raising the creative and communications industry standards in Tanzania.

Follow Us

Browse by Category

  • ! Без рубрики
  • 1
  • 2
  • 231
  • Afya Makala
  • BIASHARA
  • BURUDANI
  • Business
  • Casino
  • casino online
  • Casino UK
  • casino utan svensk licens
  • climatica.org.uk
  • curapractic-kerpen.de
  • Forex News
  • Gry
  • HABARI KIMATAIFA
  • Habari Kitaifa
  • Habari Picha
  • Kasyno Polska
  • KIMATAIFA
  • MAGAZETI
  • MAHAKAMANI
  • MAKALA
  • MAKALA AFYA
  • MAKALA-BURUDANI
  • MICHEZO
  • MICHEZO KIMATAIFA
  • MICHEZO KITAIFA
  • MICHEZO-MAKALA
  • MICHEZO-MASUMBWI
  • MITINDO
  • News
  • Nos partenaires
  • Online Kasyno
  • Post
  • Public
  • ready_text
  • RIWAYA
  • SIASA
  • Sports
  • test
  • Uncategorized

Recent News

Découvrez le Frisson des Jeux Crash d’AviaMasters

March 15, 2026

ChachaBet Official Speel & Claim 225% Bonus + Free Spins

March 15, 2026

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

No Result
View All Result

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In