SERIKALI imeanza kufuatilia kupanda gharama ya vifaa vya ujenzi ma vyakula nchini, ambapo imetoa onyo kali dhidi ya baadhi ya wafanyabiashara wanaopandisha bei kiholela.
Pia, serikali imekemea wafanyabiashara wanaopandisha gharama za mavazi kuelekea katika sikukuu za mwisho wa mwaka, ikisema inafanya ufuatiliaji ili itawachukulia hatua za kisheria.
Akizungumza na Uhuru, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, alisema kufuatia kuwepo baadhi ya wafanyabiashara wanaopandisha bei ya bidhaa mbalimbali kuelekea mwishoni mwa mwaka, serikali imeanza ufuatiliaji.
Alibainisha serikali imeanza mchakato wa kujua bei halisi ya vifaa vya ujenzi viwandani na gharama za usafi rishaji ili kupata jumla yake itakayoiwezesha kupanga bei elekezi.
Katika kukabiliana na changamoto hiyo, alisema awali Waziri (Profesa Kitila Mkumbo), alizungumza na wazalishaji wa vifaa viwandani.
Alisema katika mazungumzo hayo, wazalishaji walimhakikishia Waziri kwamba, pamoja na kupanda gharama za uzalishaji ikiwemo malighafi za chuma zinazoagizwa nje ya nchi, lakini bei ya vifaa vya ujenzi haitapanda zaidi.
Kigahe alifafanua kuongezeka maradufu bei ya vifaa kunatokana na baadhi ya wasafi rishaji hutumia fursa ya mahitaji makubwa yanayotokana na kuongezeka kwa miradi inayotekelezwa.
Aidha, alisema pamoja na kupanda kwa vifaa hivyo, hawatarajii bidhaa ya saruji itapanda kwa kuwa malighafi zote za uzalishaji wake zinatoka nchini, hivyo hakuna gharama iliyoongezeka katika mnyororo wa thamani.
“Hatutegemei saruji ipande kwa kuwa malighafi zinatoka nchini na hakuna gharama za uzalishaji zilizoongezeka, wanaopandisha ni wafanyabiashara wasio waadilifu, wanatumia mahitaji makubwa kama fursa,” alisema.
Kuhusu bidhaa mbalimbali kuelekea sikukuu, alibainisha Tume ya Ushindani (FCC) yenye jukumu la kumlinda mlaji, ilishaagizwa kufuatilia wafanyabiashara wote watakaopandisha bei za bidhaa muhimu kuelekea sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.
Alisema ufuatiliaji huo unalenga kubaini w a f a n y a b i a s h a r a watakaopandisha bei za bidhaa za viwandani kama vyakula na mavazi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao
Alieleza serikali itaendelea na jitihada za kutangaza bei elekezi kwa baadhi ya bidhaa huku akiwataka walaji kuripoti FCC iwapo watauziwa bei isiyokuwa ya kawaida.
“Tunafahamu kwamba hakuna gharama ya uzalishaji iliyoongezeka katika bidhaa kuelekea sikukuu, kupanda kwa bei kunatokana na wafanyabisahara wasiokuwa waadilifu wanaotumia mahitaji kuwa fursa,” alisema.
BEI YA VIFAA VYA UJENZI
Uchunguzi wa Uhuru katika maduka mbalimbali ya vifaa vya ujenzi umebaini nondo moja inauzwa sh. 26,000 wakati awali ilikuwa sh. 22,000. Bei ya mfuko mmoja wa saruji wenye kilogramu 50 ni sh. 16,000 kutoka sh. 14,500 ya awali.
BIDHAA ZA VYAKULA
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Kuuza na Kununua Nafaka Nchini (TAMAGRASAI), Juma Dikwe, alisema vyakula vya nafaka vimepanda bei kutokana na mvua za msimu zilizochelewa kunyesha maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza na Uhuru, alisema mchele uliokuwa ukiuzwa kilo moja sh. 1000 hadi 1700 hivi sasa unauzwa 1500 hadi 2100. Alisema bei ya maharage ya njano na kijivu, awali yaliuzwa sh. 1500 hadi 1800 hivi sasa yanauzwa 2200 hadi 2300, bei ya unga wa sembe ni sh. 1100 kutoka sh. 800 na kilo moja ya mahindi iliuzwa sh. 450 na sasa ni 670.
MAVAZI
Kwa upande wa mavazi katika maduka yaliyopo Kariakoo, Dar es Salaam, nguo moja ya mtoto wa kike kuanzia umri wa miaka mitano hadi 12 inauzwa kati ya sh. 30,000 hadi sh. 70,000.
Uhuru ilishuhudia nguo za watoto wa kiume zikiuzwa kati ya sh. 45000 hadi 80,000 kwa umri huo. Mfanyabiashara mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Elizabeth Dadishi, alisema kipindi cha kuelekea sikukuu wanapandisha bei ya mavazi ya watoto kwa kuwa ndiyo wahitaji wakubwa wa nguo.
“Kipindi hiki cha sikukuu humkuti mtu mzima anahangaika na nguo zaidi ya kumuhangaikia mtoto wake, hivyo na sisi tunapata nafasi ya kuzidisha bei kwa kuwa wanunuzi wanakuwepo,” alisema Elizabeth.
Elizabeth alisema bei ya mavazi kwa watu wazima haijazidi kwa sababu wamekuwa wateja wao wa kila siku.
“Bei ya mavazi ya nguo za watoto inapanda kila inapofi ka msimu wa sikukuu ya kwa sababu wazazi wengi hununua nguo hizo kwa msimu tofauti na ilivyo kwa watu wazima.
JUMA ISSIHAKA Na REHEMA MAIGALA