Tuesday, May 20, 2025
27 °c
Dar es Salaam
25 ° Thu
25 ° Fri
25 ° Sat
25 ° Sun
25 ° Mon
English English Kiswahili Kiswahili
UMG
  • Mwanzo
  • UMG
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara
    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
    • All
    • Sports
    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

  • Michezo
    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • MAGAZETI
    • UELEKEO
  • UMG DIGITAL
  • UELEKEO DIGITAL
    • Instagram
    • Facebook
    • Twitter
    • Youtube
  • English English
  • Kiswahili Kiswahili

No Result
View All Result
UMG
No Result
View All Result
Mwanzo SIASA

NI HISTORIA NYINGINE CCM

CCM>Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977 imekuwa ikijiimarisha

admin by admin
March 13, 2022
in SIASA
0 0
0
SHAKA ANG’AKA FAINI MIMBA ZA WANAFUNZI

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka

0
SHARES
130
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NI historia nyingine, hiki ndicho kinachojieleza baada ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), kutangaza mkakati wa kujiimarisha  kwa kuandaa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Taifa kwa ajili ya kupitisha Mapendekezo ya Marekebisho ya Katiba yake ya mwaka  1977.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977, CCM imekuwa na historia ya kujiimarisha kila mara hatua ambayo wadadisi wa kisiasa wanaiona ndiyo sababu ya kukifanya kuwa miongoni mwa vyama vikongwe imara duniani.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, katika mkutano wake na vyombo vya habari Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, ametaja moja ya sababu za marekebisho hayo ni kukiimarisha Chama.

“Juzi Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ilikutana Chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu Chamwino, jijini Dodoma kwa ajili ya kupokea taarifa kutoka kwa vitengo vya Idara za CCM  ikiwa ni hatua ya kawaida ya kujiimarisha katika utendaji  na uendeshaji wa shughuli za Chama,” ameeleza.

Shaka amesema Kamati Kuu ilipokea na kujadili pendekezo la kuitishwa kwa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Taifa.

“Katika kikao cha kawaida kilichofanyika Desemba 18, mwaka jana, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa pamoja na mambo mengine ilipokea, ilijadili na kupitisha mapendekezo ya marekebisho ya katiba  ya CCM ya mwaka 1977,Toleo la 2020,” amesema.

MALENGO YA MAREKEBISHO YA KATIBA

Shaka ameyataja malengo ya CCM kuelekea marekebisho hayo; kuwa ni kuongeza kasi na ufanisi wa kazi za Chama na utekelezaji wa maamuzi ya vikao vya Chama.

Pia, amesema ni kukiwezesha Chama kupata viongozi imara, waadilifu na wenye uwezo mkubwa katika kuongoza na kusimamia majukumu ya Serikali za Mitaa kwa ufanisi.

Tatu, Shaka amesema ni kuongeza na kuimarisha udhibiti wa Chama kwa viongozi wake wanaochaguliwa, kuongoza na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM kupitia serikali za mitaa.

Nne, amesema ni kuimarisha nguvu ya Chama katika kukabiliana na kudhibiti vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Ametaja lengo la tano, ni kuongeza uwakilishi wa Jumuia za CCM ngazi ya kata katika Mkutano Mkuu wa CCM wa Wilaya na kurekebisha itifaki ya uwakilishi unaofanana na Wenyeviti na Makatibu wa Jumuiya za CCM ngazi ya mkoa; kuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na ngazi ya Wilaya, kuwa wajumbe wa mkutano Mkuu wa mkoa.

Shaka amesema kwa  mujibu wa katiba ya CCM, mamlaka ya kupitisha na kurekebisha katiba ya Chama ipo mikononi mwa Mkutano Mkuu wa Taifa, chini ya Ibara ya 99(5) ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977, Toleo la 2020.

“Bila kuathiri uwezo wake, Mkutano Mkuu wa CCM Taifa unaweza kukiagiza kikao chochote cha CCM, kufanya kazi yoyote na Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa isipokuwa kutunga au kubadilisha sehemu yoyote ya Katiba ya Chama.

“Uchaguzi wa Wenyeviti na Makamu Makamu Mwenyekiti wa Chama,uteuzi wa mgombea wa Urais  na kumthibitisha mgonbea Urais wa Zanzibar,” alinukuu.

Amesema  katika kikao hicho, Kamati Kuu ya CCM Taifa  imeazimia  kuwasilisha kwa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, pendekezo la  kuitishwa  kwa Mkutano  Mkuu Maalumu wa CCM Taifa.

RATIBA

Shaka amesema Machi 31, mwaka huu, Kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu zitakutana.

Amesema Aprili Mosi, mwaka huu, utafanyika Mkutano Mkuu  Maalumu  wa CCM Taifa, ambapo vikao vyote vilivyotajwa vitafanyika Makao Makuu ya CCM, Dodoma.

Shaka amesema CCM imekuwa na utaratibu wa kujiimarisha nyakati zote tangu mwaka 1977 baada ya kuundwa kwake kwa vipindi tofauti imekuwa na utaratibu huo.

Alisema mwaka 1992 baada ya mfumo wa vyama vingi kurasimishwa  nchini, CCM ilijitathmini  na kujipanga na kujiimarisha upya kimuundo, kiutendaji,kiuchumi, kijamii na kimwelekeo ili kutoa fursa  ya kukidhi nyakati zilizopo.

UCHAGUZI  WA CCM

“ Mabadiliko haya ya Katiba ya CCM ni sehemu ya kujiimarisha  na kama tunavyosema tunaelekea kwenye uchaguzi, yapo maeneo ambayo kama Chama tumehisi hatujafanya vizuri, maeneo hayo tunakwenda kujiimarisha.

“ Ni kweli makatibu wa mikoa walikuwa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM lakini ikaja katikati makatibu hao wakatoka ,sasa makatibu hao wanarudi kwa sababu ya kuimarisha nguvu za Chama na tathmini ya vikao vya Chama imeona Makatibu wanapaswa kuwa sehemu ya wajunmbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,” amefafanua.

Amesema jambo la marekebisho hayo si geni, bali linaendana na matarajio ya nyakati zilizopo na kujiimarisha, huko ndipo kulipoipa fursa CCM ya kuendelea kuaminiwa kwa kupata ridhaa katika chaguzi mbalimbali kwa sababu Chama huwa kinajitathmini na kuchukua hatua ya kujiimarisha zaidi.

Shaka ameeleza kuwa, CCM tangu kuundwa kinaishi katika misingi yake na mkuu ukiwa ni katiba, kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa nyakati zote.

“Ndiyo maana tunaona kila kukicha inazidi kuimarika na inapofika wakati wa uchaguzi nafasi zote za kugombea zinakuwa katika ngazi husika ya Chama na hazuiwi mwanachama yeyote kuomba ridhaa nafasi yeyote ndani ya Chama,” alieleza.

Amesema kila mwanachama mwenye sifa, anayo haki ya kugombea nafasi yoyote ndani ya Chama.

Shaka amewataka wanachama wote wa CCM kutumia fursa ya kikatiba kuomba ridhaa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Hata hivyo, amesema katika uchaguzi huo, CCM itaendelea  kuwa kinara wa kupinga rushwa na wataufuatilia uchaguzi huo na mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa atachukuliwa hatua stahiki.

CCM ilizaliwa Februari 5, 1977 baada ya kuunganishwa Vyama vya ukombozi vya TANU na ASP.

Na ATHNATH MKIRAMWENI

admin

admin

Stay Connected test

  • 139 Follower
  • 204k Subscriber
  • 23.9k Follower
  • 99 Subscriber
  • Trending
  • Comments
  • Latest
MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

July 9, 2021
BREAKING NEWS: RATIBA LIGI KUU NBC MSIMU WA 2023/2024 HII HAPA

BREAKING NEWS: RATIBA LIGI KUU NBC MSIMU WA 2023/2024 HII HAPA

August 7, 2023
TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

July 9, 2021
BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

August 9, 2021
NDUGU MATATANI KUMSHAMBULIA, KUMJERUHI MWENZAO KISA NG’OMBE

NDUGU MATATANI KUMSHAMBULIA, KUMJERUHI MWENZAO KISA NG’OMBE

0
WAHANDISI WA HALMASHAURI WAMEKUA WAKIIKOSEA SERIKALI KWAKUTOA TAARIFA ZA UONGO

WAHANDISI WA HALMASHAURI WAMEKUA WAKIIKOSEA SERIKALI KWAKUTOA TAARIFA ZA UONGO

0

OFISA ELIMU, MHANDISI, MKUU WA SHULE WAKALIA ‘KUTI KAVU’

0
STENDI YA ZAMANI UBUNGO  KUJENGWA DEPO MABASI MWENDOKASI

STENDI YA ZAMANI UBUNGO KUJENGWA DEPO MABASI MWENDOKASI

0
TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

November 20, 2024

YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 12, 2024

November 12, 2024
YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 11, 2024

YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 11, 2024

November 11, 2024
YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 1, 2024

YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 1, 2024

October 31, 2024

Recent News

Instagram Youtube Twitter Facebook

We are a diverse team of experts, innovative thinkers, creative designers, writers, innovators, strategists, pyschologists, comunictaors and web developers. UMG is extremely passionate about growing clients’ businesses, helping them achieve their goals and making a difference by raising the creative and communications industry standards in Tanzania.

Follow Us

Browse by Category

  • Afya Makala
  • BIASHARA
  • BURUDANI
  • Business
  • HABARI KIMATAIFA
  • Habari Kitaifa
  • Habari Picha
  • KIMATAIFA
  • MAGAZETI
  • MAHAKAMANI
  • MAKALA
  • MAKALA AFYA
  • MAKALA-BURUDANI
  • MICHEZO
  • MICHEZO KIMATAIFA
  • MICHEZO KITAIFA
  • MICHEZO-MAKALA
  • MICHEZO-MASUMBWI
  • MITINDO
  • RIWAYA
  • SIASA
  • Sports
  • Uncategorized

Recent News

TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

November 20, 2024

YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 12, 2024

November 12, 2024

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

No Result
View All Result

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In