Timu ya Bunge Sports Club ya Wanaume ya Kuvuta Kamba imezigaragaza Timu za Wabunge wa Kenya na Uganda na kutwaa Ubigwa wa mchezo huo katika Mashindano ya 12 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Juba Nchini Sudan Kusini.
Timu hiyo ilitawazwa kuwa Mabingwa kwa mara ya pili mfululizo mara baada ya wenyeji Sudan Kusini kushindwa kufuatwa kanuni za Mashindano hayo katika mchezo wa fainali.