Rais wa China Xi Jinping anatarajia kufanya ziara yake ya kikazi huko Afrika Kusini wiki ijayo ambapo pia atahudhuria mkutano wa BRICS.
BRICS inasimama badala ya Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini na huonekana kama mbadala wa kundi la G7 la Mataifa yaliyoendelea. Safari ya Xi itakuwa ni ya pili ya kimataifa kwa mwaka huu, baada ya kuitembelea Urusi mwezi Machi.
Moja ya agenda kubwa za mkutano huo ni uwezekano wa kuongeza nchi wanachama wa kundi hilo.Nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Misri, Algeria na Ethiopia zimewahi kuonyesha hamu ya kujiunga.
Awali , mkutano huo ulizungukwa na maswali kama Rais wa Urusi Vladimir Putin ataweza kuhudhuria, lakini baadaye ilithibitishwa na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kuwa Putin hatodhuria. Ikiwa Putin ataondoka kwenye ardhi ya Urusi, anaweza akakamatwa kutokana na hati iliyotolewa na Makahama ya Kimataifa ya uhalifu (ICC) juu ya vita inayoendelea nchini Ukraine.
Afrika Kusini Ni mojawapo ya nchi mtiaji saini wa ICC hivyo inao wajibu wa kusaidia kumkamata.