Maafisa TEHAMA kutoka katika taasisi mbalimbali za umma wameshiriki katika kikao kazi cha kuandaa na Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao, ili kuhakikisha inaendana na Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019.
Lengo ni kuhakikisha Serikali inakua na Serikali mtandao yenye tija na inayoongeza ufanisa katika utendaji kazi na utoaji huduma kwa umma.
Kikao hicho kilichoandaliwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), kilifanyika kwa siku 3 kuanzia Agosti 15, 2023 katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijijini Dodoma.
Viwango na Miongozo hiyo inapatikana katika Tovuti ya e-GA kupitia kiungohttps://www.ega.go.tz/standards