IDADI ya watu waliofariki dunia katika Tamasha la Muziki la Supernova nchini Israel sasa imeongezeka na kufikia 260, vyombo vya habari vya nchi hiyo viliripoti, vikinukuu shirika lauokoaji la eneo hilo Zaka.
Takriban watu 3,000 waliohudhuria tamasha la usiku kucha walilengwa na Hamas kama sehemu ya shambulio kubwa la kushtukiza dhidi ya Israel.
Tamasha hilo lilifanyika katika jangwa la Negev, karibu na Kibbutz Re'im – sio mbali na Ukanda wa Gaza.
BBC