Na Mwandishi Wetu
SERIKALI ya Tanzania, imetoa wito wa kuwepo kwa amani kutokana na mzozo unaoendelea kati ya
Israel na Palestina.
Wito huo ultolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, kupitia mitandao yake ya kijamii kufuatia kuzuka kwa mgogoro huo wa Mashariki ya Kati.
Tunaziomba pande zote zinazohusika, kutafuta njia ya amani kwa mazungumzo ya kweli, yakiungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa, kwa lengo kuu la kuanzisha mataifa mawili yenye uwezo sawa na kuishi kwa maelewano alisema.