Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekabidhi Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 10,000 katika Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu na chakula katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi inayoongozwa na kauli mbiu ‘Kodi Yetu, Maendeleo Yetu, Tuwajibike’.
Misaada hiyo imekabidhiwa leo Jumatano Novemba 29,2023 na Meneja Msaidizi wa TRA Mkoa wa Shinyanga Estomihi Mossi akiwa ameambatana na Wafanyakazi wa TRA Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Tanki la kuhifadhia maji katika Hospitali ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu, Mossi amesema TRA imetoa tanki hilo ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa walipa kodi ili kupunguza changamoto ya vifaa vya kutunzia maji katika hospitali hiyo hususani katika Wodi ya Wazazi na kufulia.

”sisi TRA kila mwaka huwa tuna taratibu wa kurudisha shukrani kwa Walipa kodi kwa hiyo tunatenga wiki moja kwa mwaka kwa ajili ya kutoa shukrani kwa walipa kodi ambapo hiyo wiki inaambatana na elimu kwa walipa kodi na kutoa misaada mbalimbali. Tumekuja Kishapu kwa ajili ya kutoa msaada wa Tanki moja la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 10,000/=”,amesema.
“Tumetoa Tanki la Maji ili wagonjwa wanapokuja hapa waone kwamba hata wanapolipa kodi inarudi kuja kufanya maendeleo na kutoa huduma. Wanapoona hivyo waone umuhimu wa kulipa kodi”,ameeleza Mossi.
Katika hatua nyingine amehawamasisha wananchi kulipa kodi huku akisisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kutoa risiti na wanunuzi wa bidhaa kudai risiti.
“Kwa TRA tuna Kampeni ya Tuwajibike ambayo inawagusa watu wote wakiwemo wafanyabiashara na wanunuzi wa bidhaa. Mfanyabiashara anapouza anatakiwa ahakikishe anatoa risiti na mtumiaji wa huduma na bidhaa anatakiwa adai risiti ili serikali ipate mapato ambayo yanafanya shughuli zote za maendeleo ikiwemo ujenzi wa hospitali, vituo vya afya, barabara, huduma za elimu n.k”,amesema.