Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kutumika kwa michezo ya Ligi Kuu kwa kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.
Miundombinu ya Uwanja huo haikidhi matakwa ya kanuni kama inavyoainishwa kwenye masharti ya kanuni ya Leseni za Klabu.
Kufuatia uamuzi huo, Timu zote zinazotumia Uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutumia uwanja mwingine kama kanuni inavyoelekeza mpaka hapo Uwanja huo utakapofunguliwa tena baada ya kufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na TFF.