Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) amefanya Kikao maalum na Maafisa wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Kikomunisti Cha China tarehe 29 Aprili, 2024 Ofisi Ndogo za Makao Makuu Upanga Jijini Dar es Salaam.
Lengo na madhumuni makubwa ya kikao hicho ni kudumisha na kuimarisha uhusiano wa kimataifa na chama cha kikomunisti cha China.




























