Na Zawadi Kapambwe, Mbeya.
MKAZI wa Mwanjelwa jijini Mbeya, Martin Sinkale (39),amefikishwa mahakamani akidaiwa kuchoma nyumba ya
mama wa mkwe wake. Mshtakiwa huyo anadaiwa kuchoma nyumba hiyo kwa tuhuma za kumpokea mkewe na kuishi naye na kila alipomfuata, mama mkwe wake alimzuia kwa madai kuwa alihofia watauana.
Akitoa ushahidi wake, mlalamikaji Felista Kalinga (65), alidai kuwa kabla ya tukio la kuchomwa moto nyumba
yake, binti yake alirudi nyumbani baada ya kushindwana na mume wake.
“Mheshimiwa Hakimu, kama mzazi mwenye uchungu na binti yake, nilimpokea mwanangu na tukaendelea na
maisha, lakini cha kushangaza huyu mkwe wangu (mshtakiwa), alikuwa akija kila siku nyumbani akimuomba
mkewe arudi nyumbani kwake nami nilizuia kutokana na wao kupigana kila uchao” alidai Felista.