Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Komredi Rehema Sombi Omary (MNEC) amesema UVCCM kama taasisi chini ya Mwenyekiti wake Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) adhma yake ni Kuhakikisha inafikisha Elimu kwa Vijana kuhusu Masuala Mbalimbali ya Muungano Kila Mahali.
Ndugu Rehema Sombi amesema hayo katika Kongamano la UVCCM kuelekea Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linalofanyika Zanzibar tarehe 21 Aprili, 2024 katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani.
“Ndugu zangu Sisi Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kama Taasisi chini ya Mwenyekiti wetu Ndugu Mohammed Ali Kawaida adhma yetu ni Kuhakikisha tunafikisha Elimu kuhusu Taifa letu na Muungano kwa Vijana wenzetu Maeneo Mbalimbali nchini”
“Ndugu zangu tungesema tufanya Matembezi kama tulivyofanya kwa Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar lakini tukaona ipo haja ya kuendeleza kurithisha Elimu kuhusu Muungano wetu kwa Vijana wenzetu kuhusu Muungano wetu”.
“Tumeona Viongozi wabobezi kabisa ndio watoa mada katika Kongamano hili, nimemuona Mzee wetu Stephen Wasira, Professor Makame, na Mzee wetu Vuai Ali Vuai. Hawa wote ni Wabobezi na wameuishi Muungano wetu kwa Muda Mrefu hii inadhihirisha kuwa Elimu tunayokwenda kuipata itakwenda Kuongeza thamani ya Uzalendo katika Muungano wetu kwa Vijana wengi”. Alisema Komredi Rehema Sombi.
CC: UVCCM-Taifa.