WABUNGE Watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walioitwa mbele ya Kamati ya Maadili ya wabunge wa chama hicho wameitikia wito kwa kufika mbele ya kamati na kuhojiwa.
Wabunge hao ni aliyekuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa, ambao wamefika katika ukumbi wa makao makuu ya CCM kwa nyakati tofauti.
Akizungumza baada ya kutoka kuhojiwa Polepole (MB) amesema hawezi kuzungumza kwani utaratibu wa chama hicho kamati ndio inajukumu la kutoa taarifa.
“Utaratibu wa chama chetu kikao cha maadili ni kikao cha ndani kwahiyo taarifa zote zitatoka kwa utaratibu wa chama nawashukuruni sana,”amesema Polepole.
Na FRED ALFRED



























