MAKAMPUNI na Taasisi yaombwa kujitokeza Kudhamini Mashindano ya vijana hususan urembo ili kuwapa moyo na kutoa muamko kwa waandaji wa Mashindano hayo.
Akizungumza na Uhuru Online, Meneja Masoko wa Kinywaji chenye Kilevi, Bacardi Jason, amesema vijana wana nafasi tofauti tofauti katika jamii, lakini wakati Mwengine ni muhimu kuandaa tafrija ambazo zitaweza kujua uwezo binafsi na vipaji vya ziada vya vijana hao.
“Tunapoandaa tafrija hizo zinasaidia kuona uwezo wa vijana kama sehemu ya kipaji chake kwani ni nadra sana kuona pasipo kuandaliwa kwa matamasha ambayo yatamsukuma kuonyesha kipaji hiko mbele ya hadhira kutokana na kukutanishwa kwa watu mbalimbali mahala hapo.”
Hata hivyo Jason ameeleza kwa namna gani Kampuni hiyo inavyothamini nguvu za vijana hasa Wanamitindo pamoja na ubunifu wa Mavazi na kwa Mara nyingine Tena wanatoa udhamini kwa Jukwaa la Mbunifu wa Mitindo Remtulah 101.
“Tunathamini na kuheshimu kazi za Sanaa hivyo kwa upande wa Sanaa hii ya ubunifu wa Mavazi tumeshiriki mara kwa mara katika kutoa udhamini ili kuhakikisha linafanyika na vijana wanaonyesha vipaji vyao kwa kubuni Mavazi yao, ” amesema Jason.
Na AMINA KASHEBA