KOCHA Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha amesema mchezo wa kesho dhidi ya Kagera Sugar utachora ramani ya kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca utakaopigwa Desemba 19, 2023.
Benchikha ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumzia maandalizi ya kikosi chake watakapoikabili Kagera Sugar katika muendelezo wa ligi kuu Tanzania Bara.
Ameongeza licha ya uhitaji mkubwa wa matokeo bado ataingia kwa tahadhari kwasababu hawafahamu vizuri wapinzani wao.
“Sina taarifa za kutosha kuwahusu Kagera lakini nina fahamu ni timu nzuri,
“Tunaziheshimu timu zote ambazo tunapaswa kucheza nazo ni lazima tushinde kesho ili kutengeneza mazingira mazuri kuelekea mchezo dhidi ya Wydad.” Amesema Benchikha
Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni