Maonesho ya Wakulima yakiwa yanaendelea Jijini hapa kwenye viwanja vya Nanenane, Wakala wa usajili wa biashara na leseni(BRELA) imesajili zaidi ya Kampuni 50 kwenye maonesho hayo na kuendelea kutoa Wito kwa wananchi kuudhuria katika maonesho ili kusajili biashara zao ili kutambulika kisheria.
Aidha BRELA inaendelea kutoa msaada katika kutatua kero za wafanyabiashara kupitia huduma za usajili wa Biashara kwa watu wanaotaka kuanzisha biashara .
Afisa Kumbumbukumbu wa BRELA,Farid hoza ameeleza hayo Jijini Dodoma kwenye maonesho hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa mwananchi watakaofika katika banda hilo watapata uelewa zaidi juu ya umuhimu wa kusajili bidhaa ambazo wanazizalisha na kuziongezea ubora kwa kiwango kinachokubalika.
Katika kutoa huduma za usajili wa majina ya biashara na kampuni Afisa huyo ameeleza kuwa ni muhimu kwa kuwa inarasimisha Biashara kwa mujibu wa sheria.
“Tunatoa uwezeshi wa Huduma za Kielektroniki ambapo BRELA inatoa huduma za mtandaoni ambazo zinawezesha wananchi kufanya usajili na kufuatilia hali ya biashara zao kwa urahisi, bila mahitaji ya kufika ofisini, ” Amesema
Pamoja na hayo amezungumzia kuhusu usaidizi wa Kisheria na kueleza kuwa Wananchi wanapata ushauri kuhusu sheria za biashara, ikiwa ni pamoja na kuanzisha na kusimamia biashara kwa mujibu wa sheria zilizopo jambo ambalo husaidia kupunguza migogoro ya kisheria.
“BRELA inashughulikia usajili na urekebishaji wa taarifa za kampuni, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya majina au vikao vya uendeshaji, hivyo kurahisisha mchakato wa usimamizi wa biashara,tunatumia mifumo ya kisasa na huduma za haraka, kwa ujumla tunaimarisha uwezo wa wafanyabiashara kwa kutatua matatizo yanayohusiana na usajili wa biashara, hivyo kupunguza muda wa kusubiri na mchakato mzima kuwa rahisi zaidi, “amesema
Amesema kutokana na umuhimu wa kujisajili wamekuwa wakitembea mikoani mbalimbali kutoa elimu ambapo mpaka sasa wanufaika niwengi kwani wameshatembea takribani mikoa yote ya Tanzania pamoja na kuwafikia wakulima na wafanyabishara na bado wanaendelea kwani zoezi hilo ni endelevu.
Mmoja wa wateja wa BRELA,Yahaya Hassan amefika katioa banda hilo kufuatilia taarifa za kampuni yake huku akikiri kuwa kapata huduma nzuri na kuhudumiwa kwa haraka.
“BRELA wanatoa huduma nzuri nimefurahi kwani nisingekuja hapa kwenye maonesho ingenilazimu kusubiri kwa muda,nashauri wote wenye changamoto ya makampuni, au majina ya biashara nivyema kusongea kwenye banda ili wapate huduma kwa haraka”amesema.