Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CDE. Amos Makala amesikiliza kero za wananchi wa mji wa Mpanda kwa staili ya aina yake.
Makala ambaye ameongozana na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi katika ziara ya mikoa sita iliyoanzia Katavi, alifungua zahanati ndogo ya kusikiliza kero za wananchi wa Mpanda.
Katika kusikiliza kero hizo, Makala alikaa pamoja na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri pamoja na wakuu wa idara za serikali.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Nchimbi amesema utaratibu unaotumiwa na Makalla ni wa kisayansi.
“CCM inasikiliza kero za wananchi kisayansi” alisema Dk Nchimbi huku akishangiliwa.




























