KWA mujibu wa tovuti ya ukusanyaji wa takwimu za mitandao ya kijamii (Statista Aprili, 2019) watu milioni 23 wanatumia intaneti hapa nchini, sawa na takribani asilimia 42 ya Watanzania milioni 55.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaongoza kwa idadi kubwa zaidi ya wafuasi kwenye mitandao yote ya kijamii kati ya vyama vitano vya siasa vinavyotumia mitandao miongoni mwa vyama 19 vilivyosajiliwa nchini vinavyoonekana kuwa vinara wa kutumia kurasa za mitandao ya kijamii.