IMEELEZWA kuwa, Chanjo ya Uviko19 inayoendelea kutolewa kote nchini nikwaajili yakupunguza kasi ya maambukizi lakini pia ni Kinga dhidi ya Ugonjwa huo na sio tiba kama baadhi ya watu wanavyodhani.
Akizungumza Katika Mkutano wa wadau wa Afya na waandishi wa habari uliofanyika jijini Mwanza, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Thomas Rutachunzibwa ameeleza kuwa, dhana ya baadhi ya watu kutochanja kwa madai kuwa haisaidii chochote , ni potofu na haifai kwa jamii ya Watanzania.
Amesema kumekuwa na maswali tofauti tofauti kuhusi chanjo dhidi ya ugonjwa huo huku akiifananisha chanjo hiyo na hali halisi ya maisha ya Watanzania ambao huweka milango au kufuli kwaajili ya ulinzi wa Nyumba zao lakini vyote hivyo havizuii wezi kuiba.
“Kunawatu wanasema kwamba kwanini tunachanja na bado tunavaa Barakoa? na wataalamu wanatuambia kwamba hata ukichanja kunauwezekano wa kupata maambukizi tena, Jambo hili ni sawa na milango tunayoweka kwenye Nyumba, lakini bado wezi wanaingia hiyvo chanjo ni Kinga tu na sio tiba, hupunguza kasi ya Ugonjwa” amesema.
Ameeleza kuwa Chanjo ni bora zaidi kuliko kutochanja kwani kunapunguza kasi ya maambukizi ya Ugonjwa kwa kiasi kikubwa.
Amebainisha kuwa, mpaka sasa Mkoa wa Mwanza una takribani watu Elfu 28 waliokwisha pokea chanjo ya Uviko19 huku lengo la kitaifa likiwa ni kuchanjwa angalau kwa asilimia 60 ya Watanzania wote.
Na Blandina Aristides, Mwanza.



























