Na Mwandishi Wetu
DAKTARI Bingwa wa kwanza wa magonjwa ya moyo nchini na Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa William Mahalu, amefariki dunia.
Profesa Mahalu aliaga dunia usiku wa kuamkia juzi akipatiwa matibabu JKCI jijini Dar es Salaam katika taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk. Peter Kisenge, alitoa taarifa ya kifo cha Profesa Mahalu jana
ambaye alikuwa ni miongoni mwa mabingwa watatu wa kwanza nchini waliokwenda nje kusoma ili kutoa tiba ya kibingwa ya moyo.