Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imewatangazia Wateja wake na Wananchi wa Mikoa ya Dar es salaam na Pwani kuwa kumekuwa na ukosefu wa huduma ya maji kutokana na hitilafu katika mfumo wa gridi ya Taifa.
Maeneo yanayoathirika ni Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa Maji Ruvu Juu, Mtambo wa Maji Ruvu Chini, Mtambo wa Maji Wami, Mtambo wa maji Mtoni na Visima vya Maji Kigamboni.
“Mamlaka inategemea kuendelea na uzalishaji maji pindi huduma ya umeme itakaporejea, tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza”