MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya (DCEA), imefanikiwa kumkamata kinara (jina lake linaifadhiwa) wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya aina ya cocaine pamoja na gramu 692;336 zinazowahusisha na wengine watatu katika msako maalum unaoendelea nchini.
Mfanyanyabiashara huyo ambaye yuko kwenye orodha ya vinara wanaotafutwa duniani wa mtandao wa Cocaine alikuwa akitafutwa muda mrefu lakini DCEA walifanikiwa kumkamata eneo la Boko Wilaya ya Kinondoni na wenzake wawili wote walikamatwa jijini Dar es Salaam na mshirika wao mmoja alikamatwa kijiji cha Shamwengo Wilaya ya Mbeya vijijini, mkoani Mbeya, pamoja na washirika wake watatu ambao kati yao wawili walikamatwa jijini na
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo alisema mamlaka hiyo ilibaini kuwa wafanyabiashara wa mtandao wa coaine wamekuwa wakisafirisha dawa hizo kwa kutumia watu ambao humewa dawa hizo tumboni au kuweka kwenye mauongo mengine ya miili yao maarufu kama Punda.
“Mfanyabiashara aliyekamatwa ana mtandao mkubwa wa wabebaji (Punda) kutoka nchi mbalimbali wenye uwezo wa kubeba kati ya gramu 300,1200 hadi 2000 kwa wakati mmoja, uhalifu wake unaangukiwa katika uhalifu wa kupangwa unaovuka mipaka” alisema Kamishna Jenerali Lyimo.
Alisisitiza kwamba mamlaka hiyo inaendesha msako mkali nchi kavu na baharini kwa mwaka huu wanaofanya biashara hiyo waache mara moja kwamba Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliwawezesha kupata mafunzo mbalimbali pamoja na vifaa vya kisasa.
“Natoa onyo wafanyabiashara muache mara moja tunatangaza kabisa tunaingia kazini kupambana na wafanyabiashara wote wanaoharibu nguvu kazi ya taifa kwa kufanyabiashara ya dawa za kulevya.” Alisema