Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko, ametembelea banda la maonesho la Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick inayoendesha shughuli zake nchini kwa Ubia na Serikali kupitia Kampuni ya Twiga.
katika mkutano wa Jukwaa la Kimataifa katika Sekta ya Madini (Tanzania Mining Investment Forum) unaoendelea jijini Dar es Salaam na kupata maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni kupitia migodi yake iliyopo nchini ya Bulyanhulu, North Mara na Buzwagi, sambamba na mafanikio yaliyopatikana tangu Barrick ianze kuendesha migodi nchini.
Dk. Doto Biteko alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Samia Suluhu Hassan.
Meneja Mkuu wa Barrick nchini, Melkiory Ngido, alitoa wasilisho katika mkutano huo wa kimataifa na kubainisha mafanikio yaliyopatikana kutokana na ubia wa Barrick na Twiga nchini katika uchimbaji wa madini ambao umefanikisha kuleta mapinduzi mbalimbali yenye tija ikiwemo kutoa mchango katika pato la Taifa, kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania, kutekeleza miradi ya huduma za kijamii kupitia sera ya CSR, kuboresha sekta ya elimu sambamba na kuinua maisha ya wazabuni wa kitanzania.





























