MAKAMU wa Rais, Dk. Philip Mpango, ameondoka nchini kwenda Lilongwe, Malawi, kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Ofisi ya Makamu wa Rais, imesema mkutano huo unatarajiwa kufanyika Januari 12, 2022.
Imesema mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama, utakaoanza Januari 11, 2022.
Na Mwandishi Wetu