RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewateua makamishna wanne wa Tume ya Kurekebisha Sheria.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu wa Baraza la Mapindizi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said, imewataja makamishna hao ni Dk.Yahya Khamis Hamad na Dk. Sikujua Omar Hamdan.
Wengine ni Juma Msafiri Karibona na Salim Mohammed Abdalla na uteuzi wao umeanza Desemba 28, 2021.
Na Mwandishi Wetu



























