SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), imeiwekea ngumu Rwanda katika mchakato wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kutaka kuunda kikosi maalumu cha usalama kitakachojumuisha wanajeshi wa nchi zote wanachama.
Akizungumza mjini Kinshasa mwishoni mwa wiki iliyopita, Msemaji wa serikali ya Kinshasa, Patrick Muyaya, amesema taifa lao halitakubali wanajeshi wa Rwanda, kuwa sehemu ya kikosi cha EAC ambacho kazi yake ya kwanza inayopendekezwa na kusaidia kuleta utulivu Mashariki mwa DRC.
“Rwanda haitakubali kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kiwe na wanajeshi wa Rwanda,” alisema Msemaji wa serikali ya Kinshasa, Patrick Muyaya.
DRC inaituhumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi waliouteka mji wa Bunagana mwishoni mwa wiki iliyopita, madai ambayo tayari Rwanda imeyakanusha.