MZAZI mwenzie na msanii wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ Faima Msenga ‘Fahyma’, ametoa msimamo wake, kwamba hataki kuulizwa au kuzungumzia uhusiano wa baba mtoto wake na mpenzi wake mpya, Paula Kajala.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Fahyma ambaye pia ni mwanamitindo, amesema kwa sasa hataki kuzungumza habari za baba mtoto wake, lakini muda ukifika ataweka wazi kila kitu kuhusu uhusiano wake na Rayvan.
Mwanadada huyo alisema yeye sio mtu wa maisha ya kuigiza, hivyo anaamini mashabiki wake wanahitaji kusikia zaidi maendeleo ya kazi zake kuliko mambo mengine.
Amesema anaomba mashabiki wake kuhakikisha wanaendelea kumpa sapoti ili aendelee kufanya vizuri katika tasnia ya mitindo.
“Kwa sasa sihitaji kusikia au kuzungumzia jambo lolote kuhusiana na Rayvan na Paula, kwani nimeamua kujikita katika biashara zangu na malezi ya mtoto.
“Itakifika kipindi nitakuwa tayari mimi mwenyewe nitaweka wazi kila kitu ila kwa sasa naomba mniache.
“ Nawaomba mashabiki zangu waendelee kunipa sapoti yakutosha katika biashara zangu ili nifikie malengo niliyojiwekea,” alisema Fahyma.
Na NASRA KITANA